IOM yakabidhi Kenya magari kupiga jeki usalama mipakani

Tom Mathinji
1 Min Read
Serikali yapokea magari kutoka shirika la IOM kuimarisha usalama mipakani.

Serikali imepokea magari kutoka kwa Shrika la kimataifa la Uhamiaji (IOM), yatakayotumika kuimarisha doria za usalama katika mipaka ya taifa hili.

Magari hayo yanatarajiwa kujibu hali za dharura, na kupiga jeki juhudi za nchi hii za kukabiliana na dharura za kiusalama.

Akizungumza wakati wa hafla ya kukabidhi magari hayo leo Jumatano, katibu katika wizara ya usalama wa taifa Dkt. Raymond Omollo, alisema hatua hiyo ni motisha kubwa sana katika operesheni za kiusalama, kuimarisha usafiri, ushirikishi na kukabiliana na hatari ibuka.

Dkt. Omollo, ambaye pia ni mwenyekiti wa kamati ya operesheni na ushirikishi (BCOCC), alidokeza kuwa ushirikiano kati ya kamati ya usimamizi wa mipakani (BMS) na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), unaendelea kutekeleza wajibu muhimu katika usimamizi na usalama wa mipakani.

“Ushirikiano huu, umetekeleza maswala muhimu kama vile kutoa mafunzo kwa maafisa 395 wa mpakani kwa ushirikiano na taasisi ya mafunzo ya serikali na pia kufanikisha kuandaliwa ka kongamano la kwanza kabisa kuhusu usimamizi wa mipakani,” alisema Dkt. Omollo.

Share This Article