Maafisa wa Tume ya Kupambana na Ufisadi hapa nchini (EACC), leo Jumatatu wamemkamata mwakilishi wadi ya Huruma Peter Owera Oluoch, kwa madai ya kughushi na kutoa habari za uwongo wakati wa kujaza fomu za kujitambulisha.
Oluoch anadaiwa kuwa alitangaza ana cheti cha stashahada kutoka taasisi ya kiufundi ya Kenya Polytechnic, lakini baada ya uchunguzi ilibainika kwamba hakuwa mwanafunzi wa stashahada katika taasisi hiyo.
Wakati huo huo mwakilishi huyo wa wadi anadaiwa kughushi sahihi na muhuri kusingizia kuwa ni wakili.
Kwa sasa mshukiwa huyo anazuiliwa katika kituo cha polisi kilicho katika makao makuu ya EACC, akisubiri kufikishwa mahakamani Jumanne Machi 4,2025.
Tume ya EACC inawachunguza maafisa wa serikali kwa kughushi vyeti vyao vya masomo.