Afisa wa ardhi akamatwa Tigania Magharibi kwa tuhuma za ufisadi

Martin Mwanje
1 Min Read

Tume ya Maadili na Kupambana na Ufisadi (EACC) imemkamata Geoffrey Muchiri ambaye ni Mwanachama wa Bodi ya Udhibiti wa Ardhi katika eneo la Tigania Magharibi. 

Muchiri alikamatwa kwa tuhuma za kuitisha hongo kutoka kwa raia ili kuidhinisha masuala mbalimbali ya ardhi.

“Mshukiwa, Geoffrey Muchiri, alikamatwa na makachero wa EACC baada ya kupashwa habari na mlalamikaji aliyekuwa ameuza hekari 0.25 za ardhi na kuhitaji idhini ya bodi hiyo ili kuihamisha ardhi hiyo,” imesema EACC katika taarifa.

“Baada ya kukamatwa kwake, makachero walipata jumla ya shilingi 70,000 zinazoshukiwa kutokana na ufisadi.”

Muchiri alizuiliwa katika kituo cha polisi cha Isiolo akisubiri kufunguliwa mashtaka ya usafidi.

Share This Article