Bingwa wa zamani wa dunia wa mita 3000 kwa chipukizi chini ya umri wa miaka 20, Teresia Gateri, aliibuka mshindi wa mbio za mita 1500 katika siku ya mwisho ya mkondo wa pili wa mashindano ya cha, cha riadha Kenya yaliyoandaliwa leo katika uwanja wa manispaa ya Thika, kaunti ya Kiambu.
Gateri, akiwakilisha eneo la kati, alitumia dakika 4 sekunde 24.3 kumaliza wa kwanza, sekunde 1 mbele ya Vivian Chebet wa jeshi na Ceelestine Jepkosgei, aliyemaliza wa tatu kwa muda wa dakika 4 sekunde 27.1.
Vivian Chebet aliyeshiriki michezo ya Olimpiki mwaka jana ametwaa ubingwa wa mita 800 kwa muda wa dakika 2 na sekunde 11,akifuatwa na Vanice Kerubo wa Polisi kwa dakika 2 sekunde 13.6 ,sekunde nne mbele ya Jancinta Abese wa Magereza aliyechukua nafasi ya tatu.
Wilberforce Kones wa Polisi ameshinda mbio za moita 3,000 kuruka viunzi na maji kwa dakika 9 akifuatwa na Samuel Kiprop wa huduma ya kitaifa ya vijana NYS kwa sekunde 10.5 baadaye, huku Brian Bett wa North Rift akimaliza wa tatu kwa dakika 9 sekunde 16.1.
Daniel Kyumbe Munguti wa jeshi alisajili muda wa kasi akishinda mita 15000 kwa dakika 3 sekunde 44.5, akifuatwa na Mildan Roimet wa South Rift kwa dakika 3 sekunde 53.7.Elphas Kipkemboi, pia wa KDF, alikamilisha nafasi tatu bora kwa dakika 3 sekunde 58.6.
Boniface Mweresa alishinda mbio za mita 100 kwa kutumia sekunde 10.10, akifuatwa na Dennis Mwai na Isaac Omurwa katika nafasi za pili na tatu mtawalia.