Tuzo ya Trace ya Jux yabadilishwa kulikoni?

Awali tuzo ya Jux ilikuwa ya msanii bora nchini Tanzania lakini baadaye ikabadilishwa na kuwa msanii bora wa kiume nchini Tanzania.

Marion Bosire
1 Min Read

Mashabiki na wafuatiliaji wa muziki ndani na nje ya Tanzania wameshangazwa na mabadiliko yaliyofanywa na waandalizi wa tuzo za Trace kwa tuzo aliyoshinda msanii Juma Jux.

Awali tuzo ya Jux ilikuwa ya msanii bora nchini Tanzania lakini baadaye ikabadilishwa na kuwa msanii bora wa kiume nchini Tanzania.

Tuzo ya msanii bora wa Tanzania baadaye ilikabidhiwa mwanamuziki wa kike Faustina Charles Mfinanga, maarufu kama Nandy.

Mtangazaji Diva The Bause kupitia akaunti yake ya Instagram ametilia shaka uadilifu wa tuzo hizo za Trace kwani katika kiwango cha upigaji kura, hakukuwa na vitengo vya wasanii bora wa kike na wa kiume nchini Tanzania.

Katika kitengo kilichokuwepo awali cha msanii bora wa muziki nchini Tanzania, Jux alikuwa akipambana na Diamond Platnumz, Zuchu, Nandy, Harmonize, Marioo na Mbosso

Ikumbukwe kwamba baadhi ya tuzo hazikutolewa kwa washindi usiku rasmi wa tuzo za Trace kisiwani Zanzibar februari 26, 2025 kutokana na matatizo ya kimazingira hususan upepo mkali.

Waandalizi wa tuzo hizo za Trace wanaripotiwa kuandaa hafla nyingine ya kukabidhi washindi tuzo zao katika hoteli ya Johari Rotana jijini Dar es Salaam nchini Tanzania.

Share This Article