Donald Trump na Volodymyr Zelensky wajibizana vikali White House

Tom Mathinji
1 Min Read
Rais Donald Trump wa Marekani (kulia) na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky katika Ikulu ya White House.

Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, aliondoka Ikulu ya White House baada ya majibizano makali na Rais wa Marekani Donald Trump na Makamu wake JD Vance.

Baada ya tukio hilo lililoonyeshwa moja kwa moja kutoka White House, Rais wa Ukraine anaonekana akitoka nje ya ofisi na kuingia kwenye gari nyeusi aina ya SUV, ambalo iliondoka kwa haraka.

Muda mfupi baadaye, Trump alichapisha ujumbe kwenye mmtandao wake wa Kijamii wa Truth Social, akidai kwamba Zelensky “aliidharau Marekani katika Ofisi yake ya Oval inayopendwa. Anaweza kurejea akiwa tayari kwa mazungumzo ya amani.”

Huku hayo yakijiri Ikulu ya White House inasema Trump na Makamu wake JD Vance “hawatakubali watu wa kutumiwa vibaya”.

Katika taarifa iliyotolewa muda mfupi baada ya mkutano wao na Zelensky, Ikulu ya White House imesema wawili hao “daima watazingatia maslahi ya Wamarekani na wale wanaoheshimu nafasi ya Marekani duniani”

Share This Article