Mmoja afariki,15 wajeruhiwa kwenye ajali ya barabarani Homa Bay

Tom Mathinji
1 Min Read
Mwili waopolewa kutoka tanki la maji taka lililoporomoka Mombasa.

Mtu mmoja amefariki, huku 15 wakijeruhiwa kwenye ajali ya barabarani baada ya gari aina ya pickup iliyokuwa imewabeba watu 24 kuanguka katika kijiji cha Malongo, eneo bunge la Suba Kusini, kaunti ya Homa Bay.

Watu hao ambao ni washirika wa kanisa moja, waliokuwa wakisafiri kutoka katika hospitali ya kaunti ndogo ya Suba kuchukua mwili wa mpendwa wao, ajali hiyo ilipotokea.

Watu wanane kati yao walipata majeraha madogo na walitibiwa na kuruhusiwa kwenda nyumbani, huku waliopata majeraha mabaya wakipokea huduma za dharura katika hospitali mbali mbali za eneo hilo.

Uchunguzi wa awali umebainisha kuwa, ubebaji wa abiria kupita kiasi na hali mbaya ya barabara, zilisababisha ajali hiyo.

Maafisa wa serikali wa eneo hilo wameanzisha uchunguzi kuhusiana na ajali hiyo, wakitoa wito kwa wananchi kutosafiri wakitumia magari ya kubeba mizigo.

Share This Article