Aliyekuwa Gavana wa kaunti ya Migori Governor Okoth Obado, anatarajiwa kujitetea Mahakamani mwezi Aprili, baada ya Mahakama Kuu kuamua kuwa ana kesi ya kujibu kufuatia mauaji ya mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo, Sharon Otieno.
Obado anatarajiwa kujitetea kuanzia Aprili 23 hadi 25, 2025.
Hata hivyo, washtakiwa wenza Michael Oyamo na Caspal Obiero, watajitetea kuanzia Mei 19 hadi 23, 2025.
Hatua ya mahakama ya kumpata Obado na hatia, ilijiri baada ya upande wa mashtaka kukamilisha mawasilisho yake, ilipowawasilisha mashahidi 42, akiwemo mwana habari mmoja.
Hata hivyo, Gavana huyo alimfahamisha Lady Justice Cecilia Githua kwamba ananuia kuwasilisha ushahidi dhidi yake kupitia hati ya kiapo.
Alisema atakuwa mahakamani wakati mashahidi hao wawli watakuwa wanashuhudia.
Sharon aliuawa mwaka 2018 akiwa mja mzito, mauaji ambayo yalihushishwana Obado pamoja na washirika wake.
Watatu hao wamekanusha kuhusika kwenye mauaji hayo.