Harambee Starlets yaondoka nchini kuelekea Tunis

Dismas Otuke
1 Min Read

Timu ya taifa ya soka kwa wanawake Harambee Starlets imeondoka nchini leo jioni kuelekea mjini Tunis, Tunisia kwa mechi ya marudio raundi ya kwanza kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (WAFCON) mwaka ujao.

Starlets watakuwa na kibarua kigumu kwa mchuano huo wa marudio kesho kutwa dhidi ya wenyeji, baada ya kuambulia sare tasa nyumbani katika duru ya kwanza Jumamosi iliyopita.

Kocha Bedine Odemba, ambaye amekashifiwa vikali kutokana na uteuzi wa kikosi cha mkondo wa kwanza, ametaja kikosi cha wanandinga 23 waliosafiri kwa mchuano huo.

Makipa

Annedy Kundu, Lilian Awuor

Mabeki

Dorcas Shikobe, Enez Mango, Janet Mumo, Ruth Ingosi, Elizabeth Ochaka, Tabitha Amoit

Viungo

Corazone Aquino, Cynthia Shilwatso, Fasila Adhiambo, Lavender Akinyi, Lydia Akoth, Sheryl Angach

Washambulizi

Mwanalima Adam, Violet Nanjala, Elizabeth Wambui, Janet Bundi, Rebecca Okwaro, Elizabeth Mideva. Emily Moranga, Jentrix Shikangwa, Tereza Engesha

Mshindi wa mechi hiyo atafuzu kwa raundi ya pili atakapokutana na Gambia au Niger.

Fainali za mwaka ujao za kombe la mataifa ya Afrika WAFCON, zitaandaliwa nchini Morocco.

Kenya inawinda kufuzu kwa mara ya pili kjwa kipute hicho ilichofuzu miaka 10 iliyopita.

Share This Article