Mwanamuziki wa Marekani Jaguar Wright ametuzwa na Rais Donald Trump kutokana na juhudi zake za kufichua maovu katika tasnia ya muziki na ile ya uigizaji nchini Marekani.
Tuzo hiyo kwa jina “Defender of Freedom award” iliwasilishwa kwa Jaguar na General Michael Flynn, na inalenga kutambua kujitolea kwake kwa haki na ukweli.
Kama sauti ya kipekee na isiyoogopa katika kupambania uwazi na uwajibikaji, Jaguar ameendelea kuangazia mengi ambayo wengi wanaogopa hata kuzungumzia.
Jaguar alipokezwa tuzo hiyo katika hafla ya faragha iliyoandaliwa kwenye makazi ya Rais Trump ya Mar a Lago na alikuwa ameandamana na Liz Crokin.
Crokin naye hujihusisha na ufichuzi wa njama mbali mbali za watu maarufu nchini Marekani.
Baadhi ya ufichuzi wa Jaguar ni jinsi wadhibiti fulani wa tasnia hizo mbili nchini Marekani wananyanyasa wengine wenye talanta ambao wangependa kubobea na kuafikia ufanisi.
Wengi hawakuamini alipozungumza kuhusu sherehe ambazo P. Diddy alikuwa akiandaa mara kwa mara ambazo alikuwa akitumia kunyanyasa watu kingono na baadaye Diddy akakamatwa kwa hilo.
Aliwahi pia kusema kwamba watu wengine kadhaa maarufu wanahusika moja kwa moja kwa vitendo sawia na vya P.Diddy akiwemo Jay Z na anahisi wote pia watakamatwa na kuwajibishwa.
Kuhusu kifo cha Cathy White ambaye aliwahi kuwa mpenzi wa Jay Z, Jaguar alisema kwamba White ambaye alikuwa mjamzito kabla ya kifo chake, aliuawa na Jay Z na mkewe Beyonce na kwamba mtoto aliyekuwa akitarajia ni Blue Ivy.
Wright ambaye aliwahi kuwa mmoja wa waimbaji wasaidizi wa Jay Z, anasema kukosa kwake kutii mambo aliyotakiwa kufanya kingono ndiko kulisababisha asiendelee katika tasnia ya muziki.