Kundi haramu la Hamas limewaachilia huru mateka watatu wa Israel; Iair Horn, Sagui Dekel Chena na Sasha (Alexander) Troufanov, mapema leo katika ukanda wa Gaza.
Kwa upande wake, Israel imewaachilia huru wafungwa wa Palestina 369 kubadilishana na mateka hao.
Mpango huo ulikuwa sehemu ya makubaliano ya kusitisha mapigano katika eneo la Gaza na kurejesha amani.
Israel na Palestina ziliafikiana tarehe 19 mwezi jana kusitisha mapigano na kuwaachilia mateka wote raia wa Palestina, nayo Serikali ya Israel iwafungulie wafungwa wote raia wa Palestina walio gerezani.
Idadi hiyo inafilisha jumla ya Waisrael 19 walioachiliwa huru kufukia sasa baada ya kutekwa nyara na Hamas huku 73 wakisalia wameshikwa mateka.