Rais William Ruto na kiongozi wa ODM Raila odinga wako Adis Ababa ,Ethiopia kuhudhuria kongamano la 38 la Umoja wa Afrika AU.
Kongamano hilo litakamilika kwa uchaguzi wa mwenyekiti na anaibu mwenyekiti wa tume ya umoja wa Afrika AUC.
Raila anawania kuwa Mkenya wa kwanza kuchaguliwa mwenyekiti wa AUC .
Kiti hicho kinawaniwa na wagombeaji watatu ,James Randriamandrato kutoka Madagascar aliye na umri wa miaka 66,Ali Mahmoud Youssouf wa Djibouti mwenye umri wa miaka 65, na Raila aliye na umri wa miaka 80.
Mshindi ni sharti apate thuluthi mbili ya kura zote 49 ili kutangazwa mshindi.