Aliyekuwa mtangazaji nguli wa redio Leonard Mambo Mbotela, atazikwa leo Jumamosi katika makaburi ya Lang’ata.
Mbotela aliaga dunia wiki jana akiwa na umri wa miaka 85, baada ya kuugua kwa muda mrefu.
Misa ya Mbotela iliandaliwa jana Ijumaa katika kanisa la All Saints Cathedral Nairobi.
Mbotela alisifika sana kama miongoni mwa watangazaji wa kwanza hapa nchini huku kipindi chake maarufu cha Je, Huu ni Uungwana? kikisifika katika pembe zote za nchi.?l
Kipindi hicho kilipeperushwa katika idhaa ya KBC Radio Taifa na pia baadaye katika runinga ya KBC Channel 1.
Mambo amemwacha mjane, Alice Mwikali, na pamoja walijaaliwa watoto watatu: Jimmy Mbotela, George Mbotela na Aida Mbotela.