Waasi wa M23 wamevamia vikosi vya serikali ya jamhuri ya kidemokrasia Congo katika eneo la kusini mwa mkoa wa Kivu na kuvunja utulivu wa siku mbili za kusitishwa kwa mapigano.
Makabiliano makali yalianza jana asubuhi yapata siku tatu baada ya kongamano la marais na viongozi wa serikali za mataifa wanachama wa jumuiya ya Afrika mashariki na kusini mwa Afrika lililoafikia kukomeshwa mara moja kwa vita bila masharti.
Kundi hilo la waasi limetwaa udhibiti wa maeneo mengi mashariki mwa DRC ikiwa ni pamoja na kutwaliwa kwa mji mkuu wa eneo la mashariki wa Goma.
Msemaji wa muungano wa makundi ya waasi ikiwa ni pamoja na kundi la M23 Congo River Alliance Lawrence Kanyuka amesema waasi sasa wanalenga kutwaa mji wa Bukavu.
Takribani watu 2,900 wameuawa tangu mwanzo wa mwaka huu pekee kwenye mapigano yanayoendelea, kulingana na takwimu za umoja wa mataifa. Aidha maelfu ya wengine wamejeruhiwa huku watu laki saba wakisiwa kulazimika kuhamamakazi yao.