Kindiki: Serikali kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabia nchi

Tom Mathinji
1 Min Read
Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki.

Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki, amesema serikali imechukua hatua zifaazo kukabiliana na athari zozote za mabadiliko ya hali ya tabia nchi, yanayotarajiwa wakati wa msimu ujao.

Kindiki aliyasema hayo leo Jumanne kupitia taarifa kwenye ukurasa wake wa X, alipopokea ripoti kutoka kwa kamati tekelezi ya Bunge la Taifa kuhusiana na jinsi ya kukabiliana na ukame kutokana na hali ya hewa ya mvua ya mwezi Machi hadi Mei.

“Kenya inakabiliwa na hatari, zile za asili na zinazosababishwa na binadamu huku changamoto kuu zaidi  ikiwa ni pamoja na mafuriko na kiangazi,” alisema Prof. Kindiki.

Hata hivyo, alihakikisha kuwa  serikali inachukua hatua zote zifaazo  kukabiliana na hali hiyo.

Mamlaka ya Utabiri wa Hali ya Hewa nchini imetangaza kuwa taifa hili litapokea kiwango cha mvua kilichopungua katika miezi ya Machi, Aprili na Mei.

Share This Article