Kampuni ya Kenya Power, imeorodhesha kaunti 11 ambazo zitakosa umeme leo Jumanne ili kutoa nafasi ya kuimarishwa kwa mfumo wa usambazaji umeme.
Ukosefu huo umeme, ulianza saa mbili asubuhi na unatarajiwa kudumu hadi saa kumi na moja jioni.
Kaunti zinazoathirika ni pamoja na Nairobi, Kisumu, Siaya, Vihiga, Homa Bay, Tharaka Nithi, Nyeri, Meru, Embu, Laikipia na Mombasa.
Maeneo yaliyoathirka Nairobi ni Maji Mazuri, Chieko, Santon, Gituamba, Lucky Summer Slaughterhouse na wateja waliokaribu na sehemu hizo.
Kisumu sehemu za soko la Holo, Baga Beach, soko la Kabibi, Obambo, Camp David na Shajarand Quarry zitakosa umeme.
Huko Embu, sehemu za Privum Nuts, PCEA Muthatari, Nthokis Hotel, Itabua Secondary, Njumbiri Village, Kimangaru Market, Mikuuri, Kambo Village, Dayosisi ya Embu na NTSA Mugoya zitakuw abila umeme.
Baadhi ya sehemu za mwambao wa pwani kama vile shule ya Aldina Visram, KMTC, hospitali ya Coast General, hospitali ya macho ya Lighthouse na Barabara ya Abdel Nasser zitakosa umeme.