Naibu Rais Prof. Kithure Kindiki leo Jumatatu amefanya mashauriano na viongozi waliochaguliwa, wanataaluma na washikadau kutoka sekta mbalimbali za kiuchumi kutoka kaunti ya Samburu.
Mkutano kati yao uliofanyika katika makazi ya Naibu Rais mtaani Karen, kaunti ya Nairobi, pia uliwahusisha viongozi wa mashinani kutoka kaunti ya Samburu.

Wakati wa mkutano huo, miradi ya maendeleo inayopaswa kupewa kipaumbele katika kaunti hiyo ilijadiliwa.
Aidha ufuatiliaji wa miradi hiyo inayotekelezwa na serikali pia uliangaziwa ili kuhakikisha ufanisi katika utekelezaji wake.

Serikali ya Kenya Kwanza imeahidi kutekeleza miradi mbalimbali mwaka huu kama ilivyoelezea katika manifesto yake kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 20222 ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu kama vile barabara, madarasa shuleni na upatikanaji wa maji na afya kwa wote.