SADC yakubali kujadiliana na EAC kuhusu usalama DRC

Dismas Otuke
1 Min Read

Shirika la Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) limeitikia mwito wa kufanya majadiliano na Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) kuhusu hali ya kiusalama katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC) inayozidi kudorora kila kuchao.

Viongozi wa SADC walikutana katika kongamano lisilo la kawaida mjini Harare, Zimbabwe, na kuafikiana kuhusu haja ya kutafuta suluhu ya dharura kurejesha hali ya kawaida mjini Goma mashariki mwa DRC, ambao umetwaliwa na waasi wa M23.

Kundi la M23 limetwaa maeneo mengi ya Goma na kusababisha maelfu ya watu kutoroka makwao na mamia kuawa.

Rais Felix Tshisekedi wa DRC aliyesusia kongamano la EAC wiki hii, alihudhuria kongamano la SADC kupitia kwa njia ya mtandao.

SADC ilishinikiza kusitishwa mara moja kwa mapigano mjini Goma.

Share This Article