Mauaji ya Sharon: Gavana wa zamani Okoth Obado ana kesi ya kujibu

Martin Mwanje
1 Min Read
Okoth Obado - Gavana wa zamani wa Migori

Gavana wa zamani wa kaunti ya Migori Okoth Obado, msaidizi wake Michael Oyamo na Caspal Obiero wana kesi ya kujibu kuhusiana na mauaji ya aliyekuwa mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Rongo Sharon Otieno. 

Hii ni baada ya Jaji Cecilia Githua kubaini kuwa upande wa mashtaka umewasilisha ushahidi wa kutosha kuthibitisha kuwa watatu hao walihusika katika mauaji hayo.

Washukiwa hao walikabiliwa mashtaka mawili, la kwanza likiwa mauaji ya Sharon na la pili likihusisha mauaji ya mtoto wa Sharon ambaye alikuwa bado hajazaliwa kwani alikuwa mjamzito wakati wa mauaji yake.

Jaji Githua amewaondolea watatu hao lawama katika shtaka la pili.

Sharon aliuawa mnamo mwaka wa 2018 akiwa mjamzito katika mauaji ambayo Obado na wenzake walidaiwa kutekeleza.

Watatu hao wamekanusha kuhusika katika mauaji hayo.

 

Share This Article