Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio jana Jumanne alizungumza na Rais wa Rwanda Paul Kagame kuhusu mzozo unaoendelea katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, DRC.
Katika mazungumzo hayo, Rubio alisisitiza kuwa Marekani ina wasiwasi kutokana na mzozo unaoendelea mashariki mwa DRC, na hasa kutwaliwa kwa mji wa Goma na waasi wanaodaiwa kuungwa mkono na Rwanda wa M23.
Rubio ametaka mapigano kusitishwa mara moja kwenye eneo hilo na kwamba pande zote ziheshimu uhuru wa kimaeneo.
Rubio alihimiza kuwa lengo kuu la Marekani ni kuona amani ya kudumu inayoshughulikia masuala ya kiusalama pamoja na kuweka misingi thabiti kwa kukua kwa uchumi wa kimaeneo.