Tamasha la mwaka mpya wa jadi wa China larushwa hewani

Vyombo vya habari karibu elfu tatu kutoka nchi na maeneo zaidi ya 200 vinatangaza moja kwa moja au kuripoti kuhusu tamasha hilo.

Eric Biegon
3 Min Read
Highlights
  • Ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa kwanza ambao sasa ni 'urithi wa utamaduni usioshikika,' tamasha la mwaka mpya wa jadi la CMG limeandaa vipindi vya aina mbalimbali vikihusisha nyimbo, ngoma, opera na Wushu. Pia, watu wa kawaida kutoka sekta mbalimbali wamealikwa kuwa wahusika wakuu katika maonesho.

Tamasha la kwanza la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China larushwa hewani baada ya Sikukuu hiyo kuorodheshwa kuwa “urithi wa utamaduni usioshikika”

Tarehe 28 Januari ni mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China. Kama ilivyo desturi, saa 2 kamili usiku kwa saa za Beijing, tamasha la mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China, ambalo linaandaliwa na Shirika Kuu la Utangazaji la China (CMG) linalojulikana kama “Chunwan,” linarushwa hewani kwa ajili ya watazamaji wa kote duniani.

Vyombo vya habari karibu elfu tatu kutoka nchi na maeneo zaidi ya 200 vinatangaza moja kwa moja au kuripoti kuhusu tamasha hilo.

Mwaka mpya wa jadi wa China ni moja ya sikukuu muhimu zaidi za jadi za taifa la China, ikijumuisha maana za kitamaduni zinazohusiana na familia kujumuika, utulivu wa taifa na watu, na masikilizano kati ya binadamu na mazingira ya asili; pia ina mizizi ya kihistoria. Mwishoni mwa mwaka jana, sikukuu hiyo iliorodheshwa kama urithi wa utamaduni wa binadamu usioshikika.

Ili kusherehekea mwaka mpya wa jadi wa China wa kwanza ambao sasa ni ‘urithi wa utamaduni usioshikika,’ tamasha la mwaka mpya wa jadi la CMG limeandaa vipindi vya aina mbalimbali vikihusisha nyimbo, ngoma, opera na Wushu. Pia, watu wa kawaida kutoka sekta mbalimbali wamealikwa kuwa wahusika wakuu katika maonesho.

Tamasha hilo la mwaka huu kwa mara ya kwanza limetoa matangazo ya matoleo maalum kwa ajili ya watu wasioona na watu wasiosikia, huku likitumia mafanikio ya uvumbuzi katika teknolojia za “5G+4K/8K+Akili Bandia (AI),” na kutoa “chakula cha jioni cha kitamaduni” kwa watazamaji wa kote duniani kwa lugha 82.

Tangu mwaka 1983, kila ifikapo mkesha wa mwaka mpya wa jadi wa China, Televisheni ya Taifa ya China hufanya tamasha linalojumuisha maonesho mbalimbali ya kitamaduni. Katika miaka 42 iliyopita, kutazama tamasha hilo kumekuwa desturi mpya ya mwaka mpya wa jadi wa China baada ya kubandika karatasi za baraka, kutengeneza Jiaozi, na wanafamilia kujumuika hadi siku ya kwanza ya sikukuu na kutoa heshima kwa mababu.

Tamasha hilo linabeba hisia za kupenda nyumbani na taifa walizo nazo Wachina wote duniani, kuonyesha mvuto wa kipekee wa utamaduni wa China, na kuwa kipindi cha televisheni kinachotazamwa na watu wengi zaidi duniani wanaposherehekea ujio wa mwaka mpya.

Share This Article