Wenyeji Morocco watafungua kipute cha 35 kuwania kombe la
mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya limbukeni Comoros Disemba
21 mwaka huu katika kundi A.
Kwa mjibu wa droo iliyoundaliwa jana usiku katika ukumbi wa
Mohammed V mjini Rabat, wenyeji Atlas Lions wamejumuishwa kundi
A na The Eagles ya Mali na Chipolopolo kutoka Zambia.
Kundi B linasheheni mabingwa mara saba The Pharaohs ya Misri,
The Warriors ya Zimbabwe, Bafana Bafana ya Afrika Kusini na
Palancas Negras ya Angola.
Mabingwa mara tatu Super Eagles ya Nigeria wamo kundi C
pamoja na Uganda Cranes, Taifa Stars ya Tanzania na mabingwa wa
mwaka 2004 Carthage Eagles ya Tunisia.
Mabingwa wa mwaka 2022, Teranga Lions ya Senegal, wamo kundi D.
pamoja na the Leopards ya Jamhuri ya Kidemkorasia ya Congo, Cheetahs kutoka Benin na
Punda Milia wa Botswana.
Washindi mara mbili Desert foxes ya Algeria wamo kundi E pamoja na The Stallions
kutoka Burkina Faso, Equatorial Guinea, na Sudan huku mabingwa
watetezi Ivory Coast wakipangwa kundi F pamoja na mabingwa mara 5
Indomitable Lions ya Cameroon, The Panthers ya Gabon na Mambas
kutoka Msumbiji.
Fainali hizo zitaandaliwa katika viwanja 9 vilivyo katika miji
Sita, Kati, ya Disemba 21 na Januari 18 mwaka ujao.