Washukiwa wawili wakamatwa kwa kujisingizia kuwa maafisa wa EACC

Tom Mathinji
1 Min Read
Washukiwa wawili wakamatwa kwa kujisingizia kuwa maafisa wa EACC.

Tume ya Maadili na kukabiliana na ufisadi hapa nchini EACC, imewatia nguvuni watu wawili kwa kujisingizia kuwa maafisa wa EACC, Magharibi mwa nchi.

Wawili hao Tobias Singila Wekesa mwenye umri wa miaka 23, na Sharon Nanjala Anyango mwenye umri wa miaka 26, walikamatwa walipofika katika afisi ya ustawi wa maeneo bunge (NG-CDF), katika kaunti ya Bungoma, wakidai wanachunguza miradi inayotekelezwa na afisi hiyo.

Wanadaiwa kuitisha hongo kutoka kwa maafisa hao wa NG-CDF, wakitishia kuwachukulia hatua iwapo hawangeitikia matakwa yao.

Kulingana na tume hiyo ya EACC, Wekesa alijisingizia kuwa Mkurugenzi wa EACC kaunti ya Kakamega, wadhifa amao haupo, huku Anyango akijisingia kuwa Mkurugenzi wa EACC kaunti ya Nairobi.

Washukiwa hao wanaaminika kuwa wanafunzi wa chuo kikuu ambao hupokea fedha kwa njia za uwongo na kuwatishia waathiriwa wao.

Kwa sasa wanazuiliwa katika kituo cha polisi cha Central kaunti ya Bungoma, wakisubiri kuchukuliwa hatua zingine.

TAGGED:
Share This Article