Kocha wa Man City akiri kuwa timu ni dhaifu baada ya mechi 6 bila Ushindi

Francis Ngala
2 Min Read

Kocha wa klabu ya Manchester City Pep Guardiola amekiri kuwa wachezaji wake ni “dhaifu” baada ya kutoka sare ya mabao 3-3 na klabu ya Feyenoord, usiku wa kuamkia leo. Vijana wa Guardiola walipoteza mwelekeo na kutupa uongozi wa mabao matatu zikiwa zimesalia dakika 15 tu wakipelekea mchezo huo kuishia sare. 

Mchuano huo wa kushangaza una maana City, washindi wa Ligi ya Mabingwa 2023, wanasalia katika nafasi ya 15 katika muundo mpya wa michuano ya klabu bingwa barani ulaya, baada ya mechi ya sita katika mashindano yote bila ushindi, ikiwa ni pamoja na kushindwa mara tano.

“Tulipoteza michezo mingi hivi majuzi, sisi ni dhaifu na bila shaka, tunahitaji ushindi,” Guardiola aliambia shirika la Amazon Prime baada ya mchezoi.

Akizungumza na waandishi wa habari, Pep Guardiola alisema: “Sio kwasababu ya kutokimbia au kutojitolea, lakini soka unapaswa [kuwashwa] katika nyakati fulani kufanya hivyo. Ni vigumu kuyameza hivi sasa.”

Mechi inayofuata ya City itakuwa dhidi ya viongozi wa Ligi kuu ya Uingereza, Liverpool siku ya Jumapili. Iwapo City itapoteza mechi hiyo Anfield, kutawaacha alama 11 nyuma ya viongozi ambao ni Liverpool.

City walionekana kujiandaa kupata ushindi na kujiamini dhidi ya Feyenoord, ambao wanashikilia nafasi ya nne tu kwenye ligi ya Eredivisie ya Uholanzi, baada ya kuongoza kwa mabao matatu, huku Erling Haaland akionekana kuonyesha makali yake.

Hata hivyo, wageni waliishangaza Man City kwa kufunga mabao matatu katika robo ya mwisho ya saa – Hii ikiwa ni mara ya kwanza City kupoteza mchezo wakiwa wameongoza kwa mabao matatu chini ya Guardiola. Hakuna timu yoyote katika historia ya Ligi ya Mabingwa ambayo imekuwa ikiongoza kwa mabao matatu baada ya dakika ya 75 na kuishia kushindwa.

“Mchezo ulikuwa mzuri kwa kujiamini, tulikuwa tunacheza kwa kiwango kizuri halafu kwa mara ya kwanza kitu kilitokea, tuna matatizo.” akasema Guardiola.

Share This Article
Follow:
I am Versatile Multimedia Journalist with years of experience in Digital platforms, Live TV and Radio. In another world am a News Anchor and Reporter.