Kevin Bahati na Diana Marua wametangaza kwamba watafanya harusi tarehe 22 ila hawakutaja mwezi wala mwaka wakiacha wafuasi wao wajijazie.
Bahati alichapisha picha yao ya pamoja ambapo Diana amevaa nguo nyeupe na kubeba maua huku Bahati akiwa amevaa suti na kuandika, “Harusi yetu ya kihistoria. Tarehe rasmi 22, ebu kisia mwezi.”
Hii sio mara ya kwanza Bahati anatangaza harusi, mwaka uliopita alitangaza kwamba wangefanya harusi Disemba 12, 2023 ila haikufanyika.
Baadaye walitangaza kwamba itafanyika Oktoba 2024 tarehe ambayo tayari imepita. Bahati alimlaumu Diana akisema yeye ndiye anaahirisha harusi yao kila mara.
Wakati huo Bahati alisema Diana anapendelea harusi ya mwezi Februari na kwamba hangetangaza tarehe nyingine kwa sababu zote alizotangaza awali zimepita.
Wawili hao wamekuwa pamoja kwa muda sasa na wana watoto watatu pamoja ambao ni Majesty, Heaven na Malaika. Bahati ana binti kwa jina Mueni na mvulana mkubwa kwa jina Morgan.