Charles Okocha kufunga ndoa kesho

Marion Bosire
1 Min Read

Mwigizaji wa filamu za Nollywood nchini Nigeria Charles Okocha ametangaza kwamba atafunga ndoa kesho, Jumamosi Novemba 9, 2024.

Mwanzo alichapisha picha akiwa na mpenzi wake kwenye Instagram na kuandika”#MICHARLES2024 💍” bila maelezo zaidi.

Baadaye video inayomwonyesha akiwa kanisani na mpenzi wake katika kile kinachoonekana kuwa harusi ilivuja mitandaoni lakini hakuzungumza lolote kuihusu.

Chini ya video nyingine aliyochapisha akiwa na huyo mpenzi wake Okocha aliandika, “Uamuzi bora zaidi niliowahi kufanya!” kisha akaongeza tarehe ya kesho na kumalizia pete.

Amechapisha pia video zinazomwonyesha akigawa mialiko ya siku yake kuu kwa marafiki kama Obi Cubana na Ifeanyi Codii huku akiwatania kwamba anasubiri kwa ghamu kujiunga nao ambao tayari wameoa.

Okocha tayari ana watoto wawili na wanawake wawili tofauti.

Share This Article