Barca yaiparuza Madrid, Bernabeu katika Elclassico

Dismas Otuke
1 Min Read

Barcelona ilisajili ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Real ugenini jana usiku katika Ligi kuu nchini Uhispania,katika uga Santiago Bernabeu.

Robert Lewandowski alitikisa nyavu mara mbili huku Raphinha na Lamine Yimal wakitikisa nyavu mara moja kila mmoja.

Ilikuwa mechi ya kwanza kwa Madrid chini ya kocha Carlo Ancelloti kupoteza kwenye ligi kuu msimu huu.

Barca wanaongoza ligi hiyo baada ya mechi 11 wakiwa na alama 30 ,sita zaidi ya watani wao Madrid wanaokalia nafasi ya pili.

Share This Article