Mshukiwa mmoja wa ulanguzi wa mihadarati amekamatwa katika eneo la Malindi, kaunti ya Kilifi.
Salim Peter Katana alikamatwa nyumbani kwake katika kata ya Ngerenya wakati wa operesheni iliyoendeshwa na timu ya maafisa wa polisi usiku wa kuamkia leo Jumatatu.
Wakati wa operesheni kwenye nyumba ya mshukiwa huyo wa umri wa miaka 40, maafisa hao walipata vifurushi 38 vilivyoshukiwa kuwa na mihadarati aina ya heroine.
Mihadarati hiyo yenye uzito wa takriban kilo 3.6 inakadiriwa kuwa yenye thamani ya shilingi milioni 14.5.
Shilingi 13,000 zinazoshukiwa kutokana na mauzo ya bidhaa hiyo pia zilipatikana.
Mshukiwa alikamatwa na kupelekwa katika kituo cha polisi cha Malindi huku uchunguzi zaidi ukifanywa kwa lengo la kumfikisha mahakamani.