Comoros waigutua Tunisia nyumbani mechi ya kufuzu AFCON

Dismas Otuke
1 Min Read

Comoros waliishanagza Tunisia walipolaza bao moja kwa bila katika mechi ya kundi A, iliyochezwa mjini Tunis Ijumaa usiku.

Bao la Comoros lilipachikwa dakika ya 63 na Rafiki Said huku wakishikilia nafasi ya pili kwa alama 5, nyuma ya Tunisia wenye alama 6.

Gambia na Madagascar waliambulia sare ya bao moja katika mechi nyingine ya kundi A.

Katika kundi L,Teranga Lions waliipakata Malawi mabao manne kwa ombwe .

Mali wakiwa nyumbani Bamako waliilemea Gunea Bissau bao moja kwa bila kundi I, huku mabingwa watetezi Ivory Coast waliikung’uta Lesotho magoli 4-1 katika kundi G.

Gabon walishikwa sare tasa na Lesotho katika kundi B, nayo Angola ikiwa nyumbani ikipata ushindi wa 2-0 dhidi ya Niger mjini Luanda.

Afrika Kusini ikiwa nyumbani iliigaragaza Congo 5-0, wakati Uganda ikipata ushindi wa bao moja kwa sifuri kundi L.

Nigeria iliishinda Libya goli moja kwa bila nao Misri wakailaza Mauritania 2-0.

Share This Article