Raila aongoza mkutano wa ODM Mombasa

Dismas Otuke
0 Min Read
Kiongozi wa chama cha ODM Raila Odinga.

Kiongozi wa upinzani Raila Odinga anaongoza mkutano wa chama cha Orange Democratic Movement-ODM katika kaunti ya Mombasa.

Mkutano huo yamkini unatarajiwa kutoa mwelekeo wa chama kuhusu maswala mengi ya chama.

Yamkini mkutano huo wa siku tatu utazungumzia maswala miongoni mwao kutumuliwa kwa Naibu Rais Rigathi Gachagua na ushirikiano baina ya ODM na chama cha UDA.

Kikao hicho cha baraza kuu la ODM kilichoanza jana kitakamilika kesho.

Share This Article