Gachaguai aanza kutema ushahidi bungeni kupinga kufurushwa ofisini

Dismas Otuke
1 Min Read
Naibu Rais Rigathi Gachagua

Naibu Rais Rigathi Gachagua ameaanza kutoa utetezi na ushahidi kwenye bunge la kitaifa Jumanne jioni kupinga kutimuliwa afisini kwa tuhuma mbalimbali. 

Gachagua alianza kujitetea majira ya saa kumi na moja na dakika 19 huku akipewa muda wa saa mbili kujitetea kabla ya bunge la taifa kupiga kura ya kubaini endapo litambandua ofisini.

Naibu Rais ameanza kutoa utetezi wake dhidi ya mashtaka yote 11 yaliyowasilishwa dhidi yake.

Mashtaka hayo ni pamoja na ufisadi, matumizi mabaya ya ofisi, kueneza ukabila na kuhujumu miradi ya serikali miongoni mwa mengine.

Wabunge 291 walisaini hoja hiyo ya kumng’atua afisini Naibu Rais.

Endapo bunge la kitaifa litapitisha hoja hiyo kwa thuluthi mbili, bunge la Seneti litajadili na kupiga kura kuamua hatima ya Naibu Rais.

 

Share This Article