Jopokazi la AFC Leopards kuzuru Yanga na Simba

Dismas Otuke
1 Min Read

Jopokazi la klabu ya AFC Leopards litazuru vilabu vya Yanga na Simba vya Tanzania mwishoni mwa mwezi huu,  kufanya utathmini kuhusu mbinu bora ya kuibadilisha klabu hiyo ya jamii kuwa shirika.

Jopokazi hilo linaloongozwa na Vincent Shimoli pia linatarajiwa kuzuru matawi yote na wanachama 5,000, na wafuasi wapatao milioni sita,kupokea maoni kuhusu azma hiyo ya kubadilisha timu hiyo.

Simba na Yanga ni baadhi ya timu zinazofanya vyema katika ukanda wa Afrika mashariki na kati, tangu zibadilishe kutoka timu za kijamii hadi kuwa mashirika.

Jopokazi hilo litawasilisha mapendekezo  ya wachanama na wadau  kwa baraza kuu klabu mwezi Februari mwaka ujao, litakapowakamilisha muda wake wa kuhudumu.

Endapo kamati kuu ya Leopards itaidhinisha ripoti hiyo,inatarajiwa kuwa Ingwe, itabadilishwa kuwa kampuni ifikiapo mwishoni mwa mwaka ujao au mapema mwaka 2026.

Jopokazi hilo watu wanane linaongozwa na mwenyekiti Vincent Shimoli.

Share This Article