Wakulima Nyandarua washinikiza kuunganishiwa mabomba ya maji

Tom Mathinji
1 Min Read

Baadhi ya wakulima kutoka eneo la Ndaragwa kaunti ya Nyandarua, wametoa wito kwa viongozi wa eneo hilo kuwasaidia kuvuna maji ya mvua, wakati huu ambapo eneo hilo linashuhudia msimu wa mvua.

Kulingana na mkulima Josphat Gatu, eneo la Ndaragwa hushuhudia vipindi vya ukame na ukavu kutokana na kupakana na maeneo ya Laikipia Mashariki na Kieni, ambayo pia huwa ni maeneo kavu.

Wakulima hao sasa wanawataka viongozi wao kuwawekea maji ya mabomba kutoka mito iliyo karibu, ili kupiga jeki unyunyiziaji mashamba maji.

Walisema hatua hiyo itawawezesha kuongeza uzalishaji chakula, badala ya kutegemea maji ya mvua kwa shughuli za kilimo.

Eneo hilo limeshuhudia mvua kubwa katika muda wa mwezi mmoja uliopita, na kusababisha barabara nyingi kutopitika, huku madaraja yakiharibiwa miongoni mwa miundombinu mingine.

TAGGED:
Share This Article