Rais Ruto akutana na washindi wa medali za Olimpiki Ikuluni Eldoret

Dismas Otuke
1 Min Read

Rais William Ruto ameandaa dhifa ya staftahi mapema Alhamisi katika Ikulu ndogo ya Eldoret, kuwasherehekea  washindi wa  nishani za Olimpiki katika makala  ya Paris yaliyokamilika Jumapili iliyopita.

Kenya ilimalzia ya 17 katika msimamo wa dunia kwa dhahabu 4 fedha 2 na shaba tano  huku, ikiibuka bora barani Afrika katika mashindano hayo ya Olimpiki.

Ni mara  ya kwanza kwa Rais Ruto kuwalaki wanariadha katika Ikulu ya Eldoret .

Beatrice Chebet alishinda dhahabu mbili katika mita 5,000 na 10,000 huku Faith Kipyegon akitwaa dhahabu ya mita 1,500 naye Emmanuel Wanyonyi katika mita 800.

Faith Kipyegon na  Ronald Kwemoi walishinda medali za fedha katika  mita 5,000 .

Faith Cherotich,Abraham Kibiwott,Hellen Obiri,Benson Kipruto  na Mary Moraa walinyakua nishani za  shaba.

Rais Ruto ameandamana na naibu wake Rigathi Gachagua na Spika wa Bunge la Kitaifa Moses Wetangula.

Share This Article