Mitihani ya kitaifa kuathiriwa kutokana na kupunguzwa kwa bajeti

Dismas Otuke
1 Min Read
Katibu katika idara ya Uhamiaji Dkt. Belio Kipsang.

Katibu wa Elimu  ya msingi Belio Kipsang ameonya kuwa huenda mitihani ya kitaifa ikaathiriwa vibaya, kutokana na hatua ya serikali ya kupunguza bajeti ya wizara hiyo.

Kipsang amesema watahiniwa wapatao milioni 2.3 wanaotazamiwa kukalia mitihani ya kitaifa mwaka huu huenda wakaathiriwa na kupunguzwa kwa bajeti ambayo itavuruga mchakato mzima wa mitihani ya kitaifa.

Serikali imekata shilingi bilioni 14.9 za wizara ya elimu zikiwemo bilioni 8 za matumizi ya kila siku na nyingine bilioni 6.9 za kugharimia maendeleo katika wizara hiyo huenda kukatatiza utoaji huduma.

Kulingana na agizo hilo pia mpngp wa lishe shuleni ambao ulikuwa umetengewa shilingi bilioni tatu utaathiriwa  baada ya bajeti yake kuondolewa na kuelekezwa kwingine.

Share This Article