Mshindi wa nishani ya fedha ya mita 400 barani Afrika Kevin Kipkorir hatimaye atajiunga na wenzanke kambini huko Miramas nchini Ufaransa kujiandaa kwa michezo ya Olimpiki.
Kulingana naibu kiongozi wa ujumbe wa Kenya Barnaba Korir,mwanariadha huyo alikuwa ameondolewa katka kikosi cha Kenya kwa kukosa kutimiza masharti ya kitengo cha maadili ya wanariadha AIU kuhusu vipimo vya ulaji muku.
Kipkorir alikuwa amepimwa mara nne dhidi ya laji muku katika muda wa siku 18 badala ya siku 21 inavyohitajika hali iliyochangia kuondolewa kwake katika timu ya mita 400 kwa wanariadha wanne kupokezana kijiti.
Hata hivyo viongozi wa ujumbe wa Kenya kwa Olimpiki wamemruhusu ajiunge na wenzake kambini mjini Miramas Ufaransa huku wakisubiri rufaa ya kumruhusu ashiriki mashindanoni.
Makala ya 33 ya michezo ya Olimpiki yatang’oa nanda tarehe 26 mwezi huu na kuendelea hadi tarehe 11 mwezi ujao.