Rais William Ruto anatarajiwa kukutana na vijana wa Gen Z kupitia kwa mtandao wa X-Space, ili kujadili maswala yaliyoibuliwa na vijana hao wakati wa maandamani ya kitaifa yaliyodumu kwa majuma mawili.
Kikao hicho ambacho pia kitahudhuriwa na baraza zima la Mawaziri kimeratibiwa kuanza saa nane adhuhuri na kukamilika saa kumi na moja jioni.
Itakuwa ni mara ya kwanza tangu kuanza kwa maandamano ya kupinga mswada wa fedha yaliyoongozwa na vijana hao.
Vijana hao walilazimika kufutilia mbali maandamano ya jana baada ya shughuli hiyo kuingiliwa na magenge ya majambazi ambayo yamekuwa yakipora mali na kusababisha uharibifu .