Wenyeji Ujerumani ndani ya raundi ya pili michuano ya Euro

Dismas Otuke
1 Min Read

Waandalizi wa makala ya 17 ya fainali za kuwania kombe la bara Ulaya Ujerumani, wamefuzu kwa hatua ya mwondoano baada ya kusajili ushindi wa pili kundini A Jumatano usiku walipowaadhibu Hungary mabao 2 kwa bila.

Jamal Musiala  na nahodha İlkay Gündoğan  walifunga dakika za 22 na 67 mtawalia kuwapa mabingwa hao mara tatu ushindi uliowafuzisha kwa raundi ya pili wakiwa na pointi sita.

Kwenye mtanange mwingine wa kundi A, Scotland na Uswizi walitoshana nguvu ya bao moja kwa moja uwanjani RheinEnergie.

Scott McTominay aliiweka Scotland mbele  kunako dakika ya 13 kisha Xherdan Shaqiri akakomboa dakika ya 26.

Kundini  B  Croatia yake Luka Modric  ilitoka sare ya mabao 2 dhidi ya  Albania.

Croatia na Albania zilipoteza mechi za mwanzo dhidi ya Uhispania na Italia mtawalia na ambazo zitamenyana leo saa nne usiku.

Mechi nyngine za leo saa kumi jioni na saa moja usiku ni za kundi C.

Slovenia watazichapa dhidi ya  Serbia kisha Denmark wakabane koo na Uingereza.

TAGGED:
Share This Article